19Wewe wajua kulaumiwa kwangu, kuaibishwa kwangu, na kudharauliwa kwangu; wapinzani wangu wote wako mbele yako.
20Lawama imevunja moyo wangu; nimejawa na huzuni kubwa; nilitafuta mtu wa kunihurumia, lakini hakuwepo; nilitafuta wafariji, lakini sikupata.
21Walinipa sumu kwa ajili ya chakula changu; katika kiu yangu walinipa siki ninywe.
22Meza yao mbele yao na iwe mtego; wafikiripo wako kwenye usalama, iwe kitanzi.
23Macho yao na yatiwe giza ili kwamba wasiweze kuona; uvifanye viuno vyao kutetemeka daima.