Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 58

Zaburi 58:3-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Waovu huenenda katika upotovu hata walipokuwa tumboni; wao wanaenenda katika upotovu tangu kuzaliwa, wakiongea uongo.
4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka; wako kama fira kiziwi azibaye masikio yake,
5ambaye hasikilizi sauti ya waganga, haijalishi ustadi walio nao.
6Vunja meno yao midomoni mwao, Mungu; uyatoe meno ya mwana simba, Yahwe.
7Wayeyuke kama maporomoko ya maji; wafyatuapo mishale yao, iwe kama haina ncha.
8Wawe kama konokono ambaye huyeyuka na kutoweka, kama mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati ambaye hakuona jua.
9Kabla ya vyungu vyenu kupata joto la kuungua kwa miiba, yeye ataviondosha kwa upepo mkali, miiba ya kijani yote na ile inayoungua.
10Mwenye haki atafurahia atakapoona kisasi cha Mungu; ataiosha miguu yake kwenye damu ya waovu,
11hivyo watu watasema, “Hakika kuna tuzo kwa ajili ya mtu wenye haki; hakika kuna Mungu ahukumuye ulimwengu.”

Read Zaburi 58Zaburi 58
Compare Zaburi 58:3-11Zaburi 58:3-11