Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 55

Zaburi 55:5-16

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Uwoga na kutetemeka kumenijia, nayo hofu imenielemea.
6Nikasema, “Oh, kama tu ningekuwa na mabawa kama njiwa! Ningelipaa mbali na kupata pumziko.
7Tazama, ningeenda mbali; ningekaa jangwani. Selah
8Ningefanya haraka kuja mafichoni mwako kuzikimbia dhoruba na tufani.”
9Uwaangamize, Bwana, vuruga lugha zao! Kwa maana nimeona vurugu na ugomvi katika mji.
10Mchana na usiku wao huenda kwenye kuta zake; uchafu na ufisadi uko katikati yake.
11Uovu uko katikati yake; ukandamizaji na uongo hauiachi mitaa yake.
12Kwa maana hakuwa adui aliye nikemea, hivyo ningevumilia; wala ingekuwa ni yule aliye nichukia aliyejiinua mwenyewe dhidi yagu, hivyo ningejificha asinione.
13Lakini ulikuwa wewe, mtu sawa na mimi, mwenzangu na rafiki yangu.
14Tulikuwa na ushirika mtamu pamoja; tuliingia katika nyumba ya Mungu tukiwa na umati mkubwa.
15Kifo na kiwapate ghafla; na washuke wakiwa hai kuzimuni, maana ndiko waishiko waovu, hapo hapo kati yao.
16Lakini kwangu mimi, nitamwita Mungu, na Yahwe ataniokoa.

Read Zaburi 55Zaburi 55
Compare Zaburi 55:5-16Zaburi 55:5-16