Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 55

Zaburi 55:18-22

Help us?
Click on verse(s) to share them!
18Kwa usalama kabisa atayaokoa maisha yangu na vita dhidi yangu, kwa maana wale waliopigana nami walikuwa ni wengi.
19Mungu, yule unayetawala milele, atawasikia na kuwaaibisha wao. Selah Hawabadiliki, na hawamhofu Mungu.
20Rafiki yangu ameinua mikono yake dhidi ya wale waliokuwa na amani naye; Hakuheshimu agano alilokuwa nalo.
21Mdomo wake ulikuwa laini kama siagi, lakini moyo wake ulikuwa adui; maneno yake yalikuwa laini kuliko mafuta, lakini yalikuwa ni panga zilizochomolewa.
22Umtwike mizigo yako Yahwe, naye atakusaidia; yeye hataruhusu mtu mwenye haki kuyumbayumba.

Read Zaburi 55Zaburi 55
Compare Zaburi 55:18-22Zaburi 55:18-22