Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 51

Zaburi 51:3-17

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
4Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.
5Tazama, nilizaliwa katika uovu; pindi tu mama yangu aliponibeba mimba, nilikuwa katika dhambi. Tazama, wewe unahitaji uaminifu ndani ya moyo wangu;
6katika moyo wangu wewe utanifanya niijue hekima.
7Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.
8Unifanye kusikia furaha na shangwe ili kwamba mifupa ulioivunja ifurahi.
9Uufiche uso wako mbali na dhambi zangu na uyafute maovu yangu yote.
10Uniumbie moyo safi, Mungu, na uifanye upya roho ya haki ndani yangu.
11Usiniondoe uweponi mwako, na usimuondoe roho Mtakatifu ndani yangu.
12Unirudishie furaha ya wokovu wako, na unihifadhi mimi kwa roho ya utayari.
13Ndipo nitawafundisha wakosaji jia zako, na wenye dhambi watakugeukia wewe.
14Unisamehe kwa ajili ya umwagaji damu, Mungu wa wokovu wangu, nami nitapiga kelele za shangwe ya haki yako.
15Ee Bwana, uifungue midomo yangu, na mdomo wangu itazieleza sifa zako.
16Kwa maana wewe haufurahishwi katika sadaka, vinginevyo ningekutolea sadaka; wewe hauwi radhi katika sadaka ya kuteketezwa.
17Sadaka ya Mungu ni roho iliyovunjika. Wewe, Mungu hautadharau moyo uliopondeka na kujutia.

Read Zaburi 51Zaburi 51
Compare Zaburi 51:3-17Zaburi 51:3-17