Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 51

Zaburi 51:1-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Unirehemu, Mungu, kwa sababu ya uaminifu wa agano lako; kwa ajili ya wingi wa matendo yako ya rehema, uyafute makosa yangu.
2Unioshe kabisa uovu wangu na unisafishe dhambi zangu.
3Kwa maana ninayajua makosa yangu, na dhambi yangu iko mbele yako siku zote.
4Dhidi yako, wewe pekee, nimetenda dhambi na kufanya uovu mbele ya macho yako; uko sawa usemapo; wewe uko sahahi utoapo hukumu.
5Tazama, nilizaliwa katika uovu; pindi tu mama yangu aliponibeba mimba, nilikuwa katika dhambi. Tazama, wewe unahitaji uaminifu ndani ya moyo wangu;
6katika moyo wangu wewe utanifanya niijue hekima.
7Unisafishe kwa hisopo, nami nitakuwa safi; unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.

Read Zaburi 51Zaburi 51
Compare Zaburi 51:1-7Zaburi 51:1-7