Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 4

Zaburi 4:4-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Tetemekeni na kuogopa, lakini msitende dhambi! Tafakarini mioyoni mwenu kwenye vitanda vyenu na muwe kimya.
5Toeni matoleo ya haki na muweke imani yenu katika Yahweh.
6Wengi husema, “Ni nani atakaye tuonyesha chochote kilicho kizuri?” Yahweh, utuangazie nuru ya uso wako.
7Umeupa moyo wangu furaha kuu kuliko wao wanapozidishiwa nafaka na divai mpaya.
8Ni amani kuwa nitajilaza na kusinzia, kwako pekee, Yahweh, nifanye kuwa salama kabisa.

Read Zaburi 4Zaburi 4
Compare Zaburi 4:4-8Zaburi 4:4-8