Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 49

Zaburi 49:8-20

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
9Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
10Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
11Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
12Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
13Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa,...
14Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao.
15Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. Selah
16Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.
17Maana atakapo kufa hataondoka na chochote; utukufu wake hautamfuata yeye.
18Yeye huifurahisha nafsi yake awapo hai na watu hukusifu wewe uishipo maisha yako mwenyewe-
19naye atakwenda kwenye ukoo wa baba zake naye kamwe hataiona nuru tena.
20Yule ambaye ana mali lakini hana ufahamu ni kama wanyama, ambao wataangamia.

Read Zaburi 49Zaburi 49
Compare Zaburi 49:8-20Zaburi 49:8-20