Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 44

Zaburi 44:2-8

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Uliwafukuza mataifa kwa mkono wako, lakini ukawafanya watu wetu kuishi humo; wewe uliwataabisha mataifa, lakini ukawaeneza watu wetu katika nchi.
3Kwa maana hawakupata umiliki wa nchi kwa upanga wao, wala mkono wao wenyewe haukuwaokoa; bali mkono wako wakuume, mkono wako, na nuru ya uso wako, na kwa sababu uliwaridhia.
4Mungu, wewe ni Mfalme wangu, amuru ushindi kwa ajili ya Yakobo.
5Kwa uweza wako tutawaangusha chini maadui zetu; kwa jina lako tutatembea juu yao, wale wanao inuka dhidi yetu.
6Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
7Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
8Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. Selah

Read Zaburi 44Zaburi 44
Compare Zaburi 44:2-8Zaburi 44:2-8