16kwa sababu ya sauti yake iliyo kemea na kutukana, kwa sababu ya adui na kisasi.
17Yote haya yametupata sisi; bado hatukukusahau wewe wala kulikosea agano lako.
18Mioyo yetu haikukengeuka; hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19Bali wewe umetuadhibu vikali katika mahali pa mbweha na kutufunika na uvuli wa mauti.
20Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kueneza mikono yetu kwa Mungu mgeni,
21Mungu asingeligundua hili? Kwa maana yeye anazijua siri za moyo.
22Hakika, kwa ajili ya jina lako tutauawa siku zote; tunahesabiwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.