Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 41

Zaburi 41:4-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Nami nilisema, “Yahwe unihurumie! Uniponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe.”
5Adui zangu huongea maovu dhidi yangu, wakisema, 'Atakufa lini na jina lake lipotee?'
6Adui yangu ajapo kuniona, huongea mambo yasiyo na maana; moyo wake hukusanya maafa yangu kwa ajili yake mwenyewe; na aondokapo kwangu, yeye huwaambia watu wengine kuhusu hayo.
7Wale wote wanaonichukia kwa pamoja hunon'gona dhidi yangu; nao wanafarijika kwa ajili ya maumivu yangu.
8Wakisema, “Gonjwa baya limemshikilia yeye haswa; na sasa kuwa amelala kitandani, hatainuka kamwe.”
9Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.
10Bali wewe, Yahwe, unihurumie na uniinue ili kwamba niwalipizie kisasi.
11Na hivi nitajua kuwa unafurahishwa nami, kwa kuwa adui yangu hatafurahia kunishinda.
12Kwangu mimi, wewe unanisaidia katika uadilifu wangu na utaniweka mbele ya uso wako milele.

Read Zaburi 41Zaburi 41
Compare Zaburi 41:4-12Zaburi 41:4-12