Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 39

Zaburi 39:2-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
2Nilikaa kimya; Nilizuia maneno yangu hata kuongea lolote zuri, na maumivu yangu yalizidi sana.
3Moyo wangu ukawaka moto; nilipoyatafakari mambo haya, yaliniunguza kama moto. Ndipo mwishowe niliongea.
4Yahwe, unijulishe ni lini utakuwa mwisho wa maisha yangu na kiwango cha siku zangu. Unioneshe jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.
5Tazama, wewe umezifanya siku zangu kama upana wa kiganja changu tu, sikuzangu za kuishi ni kama si kitu mbele zako. Hakika kila mtu ana pumzi moja. Selah
6Hakika kila mtu hutembea kama kivuli. Hakika kila mmoja hufanya haraka kuhusu kukusaya utajiri ingawa hawajui ni nani atazipokea.
7Sasa, Bwana, ninasubiri kwa ajili ya nini? Wewe ni tumaini langu pekee.
8Uniokoe na dhambi zangu; usinifanye laumu ya wabumbavu.
9Niko kimya na siwezi kufungua mdomo wangu, kwa sababu ni wewe ndiwe umefanya hivyo.
10Acha kunijeruhi; nimezidiwa na pigo la mkono wako.
11Wewe unapowaadhibu watu kwa ajili ya dhambi, huvila kama nondo vitu vyao wavitamanivyo; hakika watu si kitu bali mvuke. Serah

Read Zaburi 39Zaburi 39
Compare Zaburi 39:2-11Zaburi 39:2-11