Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 35

Zaburi 35:1-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Yahwe, uwashughulikie wale wanao nishughulikia mimi; upigane nao wanao pigana nami.
2Uikamate ngao yako ndogo na ngao kubwa; inuka unisaidie.
3Uutumie mkuki wako na shoka lako la vita kwa wale wanao nifukuzia; uuambie moyo wangu, “Mimi ni wokovu wako.”
4Waaibishwe na kudharauliwa wale wanaoutafuta uhai wangu. Warudishwe nyuma na wafedheheshwe wanao panga kunidhuru.
5Wao wawe makapi mbele ya upepo, malaika wakiwafutilia mbali.
6Njia yao na iwe giza na utelezi, malaika wa Yahwe wakiwafukuzia.
7Wamenitegea mtego bila sababu; bila sababu wamechimba shimo kwa ajili ya uhai wangu.
8Uharibifu na uwapate wao kwa kushitukiza. Mtego ambao wameutega na uwanase wao. Na wadumbukie humo, ili kwamba waangamizwe.
9Bali mimi nitakuwa nafuraha ndani ya Yahwe na ndani ya wokovu wake.
10Mifupa yangu yote itasema, “Yahwe, ni nani kama wewe, uokoaye walio onewa mkononi mwa walio na nguvu kuwazidi wao na masikini na wahitaji mkononi mwa wale wanaojaribu kuwaibia?”
11Mashahidi wa uongo wamesimama; wananishitakia uongo.
12Kwa ajili ya wema wananilipa mabaya. Nina huzuni nyingi.
13Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
14Nilienenda katika huzuni kana kwamba walikuwa ni ndugu zangu; niliinama chini nikiomboleza kana kwamba ni kwa ajili ya mama yangu.

Read Zaburi 35Zaburi 35
Compare Zaburi 35:1-14Zaburi 35:1-14