Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 34

Zaburi 34:3-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake.
4Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.
5Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
6Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
7Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
8Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
9Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
10Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
11Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.

Read Zaburi 34Zaburi 34
Compare Zaburi 34:3-11Zaburi 34:3-11