Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 25

Zaburi 25:9-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
9Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
10Njia zote za Yahwe ni za upendo wa kudumu na niaminifu kwa wote wanao tunza agano na maagizo ya amri zake.
11Kwa ajili ya jina lako, Yahwe, unisamehe dhambi zangu, kwa kuwa ni nyingi mno.
12Ni nani ambaye anamuogopa Yahwe? Bwana atamfundisha yeye katika njia ambayo anapaswa kuichagua.
13Maisha yake yataenenda katika uzuri; na uzao wake utairithi nchi.
14Urafiki wa Yahwe ni kwa ajili ya wale wanao mheshimu yeye, naye hulifanya agano lake lijulikane kwao.
15Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
16Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
17Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
18Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
19Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.
20Uyalinde maisha yangu na uniokoe; usiniache niaibishwe, Kwa kuwa kwako nakimbilia usalama!
21Uadilifu na unyofu vinihifadhi, kwa kuwa nina kutumainia wewe.

Read Zaburi 25Zaburi 25
Compare Zaburi 25:9-21Zaburi 25:9-21