Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 22

Zaburi 22:25-31

Help us?
Click on verse(s) to share them!
25Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
26Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
27Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
28Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa.
29Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe.
30Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana.
31Wao watakuja na kuzungumza kuhusu haki yake; wao watawaambia watu ambao bado hawaja zaliwa yale ambayo Yahwe ameyafanya!

Read Zaburi 22Zaburi 22
Compare Zaburi 22:25-31Zaburi 22:25-31