Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 19

Zaburi 19:8-13

Help us?
Click on verse(s) to share them!
8Maelekezo ya Yahwe ni ya hakika, yakiufanya moyo kuwa na furaha; amri ya Yahwe ni safi, ikileta mwanga kwenye macho yetu.
9Hofu ya Yahwe ni safi, inadumu milele; amri za haki ya Yahwe ni za kweli na zote ni za hakika!
10Nazo zina thamani kuliko dhahabu, nazo ni tamu kuliko asali na matone ya asali kutoka sega la asali (sega la nyuki).
11Ndiyo, kupitia hizo mtumishi wako anaonywa; na katika kuziamini kuna thawabu.
12Ni nani ambaye aweza kuyatambua makosa yake yote mwenyewe? Unitakase makosa yaliyo fichika.
13Pia umuepushe mtumishi wako na dhambi za majivuno; usiziruhusu kunitawala. Ndipo nitakuwa mkamilifu, na mimi sitakuwa na hatia ya makosa mengi.

Read Zaburi 19Zaburi 19
Compare Zaburi 19:8-13Zaburi 19:8-13