Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 17

Zaburi 17:3-14

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Kama utaujaribu moyo wangu, kama utakuja kwangu wakati wa usiku, wewe utanitakasa na hautapata mipango yeyote ya uovu; mdomo wangu hautavunja sheria.
4Kama kwa matendo ya binadamu, ni katika neno la midomo yako ya kuwa nimejiepusha na njia za wahalifu.
5Mwenendo wangu umeshikila kwa umakini mwenendo wako; miguu yangu haija teleza.
6Nakuita wewe, kwa kuwa unanijibu, Mungu; geizia sikio lako kwangu na usikilize ninapo ongea.
7Onyesha uaminifu wa agano lako katika namna ya ajabu, wewe uokoaye kwa mkono wa haki yako wale wanao kukimbilia wewe kutoka kwa adui zao.
8Unilinde kama mboni ya jicho lako; unifiche katika kivuli cha mbawa zako
9kutoka katika uwepo wa waovu ambao wananitusi, adui zangu wanizungukao.
10Wao hawana huruma kwa yeyote; midomo yao huongea kwa majivuno.
11Wao wame zizunguka hatua zangu. Wamekaza macho yao wanishambulie mpaka ardhini.
12Wao ni kama mfano wa hasira ya simba mawindoni. Ni kama simba kijana anapotokea mafichoni.
13Inuka, Yahwe! Uwashambulie! Uwaangushe chini kwenye nyuso zao! Uyaokoe maisha yangu kutokana na waovu kwa upanga wako!
14Uniokoe kutoka kwa watu hawa kwa mkono wako, Yahwe, kutoka kwa watu wa dunia hii ambao utajiri wao ni maisha haya pekee! Wewe utayajaza matumbo ya wale uwathaminio na utajiri; watakuwa na watoto wengi na wataacha utajiri wao kwa watoto wao.

Read Zaburi 17Zaburi 17
Compare Zaburi 17:3-14Zaburi 17:3-14