Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 147

Zaburi 147:12-19

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni.
13Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
14Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
15Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.
16Huifanya theluji kama sufu, huitawanya barafu kama majivu.
17Hutupa mvua ya mawe kama makombo, ni nani awezaye kuhimili baridi aitumayo?
18Hutuma amri zake na kuziyeyusha, huvumisha upepo wake na hutiririsha maji.
19Hutangaza neno lake kwa Yakobo, amri zake na hukumu zake kwa Israeli.

Read Zaburi 147Zaburi 147
Compare Zaburi 147:12-19Zaburi 147:12-19