Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 147

Zaburi 147:1-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Msifuni Yahwe, kwa maana ni vyema kumwimbia sifa Mungu wetu, ni kuzuri, kusifu kwa faa sana.
2Yahwe huijenga tena Yerusalemu, huwakusanya pamoja watu wa Israeli waliotawanyika.
3Huponya mioyo iliyopondeka na kuganga majeraha yao.
4Huzihesabu nyota, naye huzipa majina zote.
5Ukuu ni wa Bwana wetu na nguvu zake ni za kutisha, ufahamu wake hauwezi kupimika.
6Yahwe huwainua wanyonge, huwashusha chini wenye jeuri.
7Mwimbieni Yahwe kwa shukurani, mwimbieni sifa Mungu wetu kwa kinubi.
8Huzifunika mbingu kwa mawingu na huiandaa mvua kwa ajili ya nchi, akizifanya nyasi kukua juu ya milima.
9Huwapa wanyama chakula na wana kunguru waliapo.
10Hapati furaha katika nguvu ya farasi, wala haridhii miguu imara ya mwanadamu.
11Yahwe huridhia katika wale wanao muheshimu yeye, watumainio katika uaminifu wa agano lake.
12Msifuni Yahwe, Yerusalemu, msifuni Mungu wenu, Sayuni.
13Maana yeye huyakaza mapingo ya malango yako, huwabariki watoto wako kati yako.
14Huletamafanikio ndani ya mipaka yako, hukutosheleza kwa ngano bora.
15Huipeleka amri yake juu ya nchi, amri zake hupiga mbio sana.

Read Zaburi 147Zaburi 147
Compare Zaburi 147:1-15Zaburi 147:1-15