Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 145

Zaburi 145:3-15

Help us?
Click on verse(s) to share them!
3Yahwe ndiye mkuu na wakusifiwa sana; ukuu wake hauchunguziki.
4Kizazi kimoja kitayasifu matendo yako kwa kizazi kijacho na kitatangaza matendo yako makuu.
5Nitaitafakari fahari ya utukufu wa adhama yako na matendo yako ajabu.
6Watanena juu ya nguvu ya kazi zako za kutisha, nami nitatangaza ukuu wako.
7Nao watatangaza wingi wa wema wako, na wataimba kuhusu haki yako.
8Yahwe ni wa neema na huruma, si mwepesi wa hasira na mwingi katika uaminifu wa agano lake.
9Yahwe ni mwema kwa wote; huruma zake zi juu ya kazi zake zote.
10Vyote ulivyo viumba vitakushukuru wewe, Yahwe; waaminifu wako watakutukuza wewe.
11Waaminifu wako watanena juu ya utukufu wa ufalme wako, na watahubiri juu ya nguvu zako.
12Watayafanya matendo makuu ya Mungu ya julikane na wanadamu na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13Ufalme wako ni wa milele, na mamlaka yako ya dumu kizazi hata kizazi.
14Yahwe huwategemeza wote waangukao na huwainua wote walioinama chini.
15Macho ya wote yanakungoja wewe; nawe huwapa chakula chao kwa wakati sahihi.

Read Zaburi 145Zaburi 145
Compare Zaburi 145:3-15Zaburi 145:3-15