Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 142

Zaburi 142:1-6

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kwa sauti yangu namlilia Yahwe anisaidie; kwa sauti yangu naomba kwa ajili ya neema ya Yahwe.
2Namwaga malalamiko yangu mbele zake; ninamwambia shida zangu.
3Roho yangu inapokuwa dhaifu ndani yangu, wewe unajua mapito yangu. Kwenye njia niipitayo wamenifichia mtego.
4Natazama kulia kwangu na sioni yeyote anayenijali. Sina pa kukimbilia; hakuna anayejali kuhusu uhai wangu.
5Nilikuita wewe, Yahwe; nikasema, “Wewe ni kimbilio langu, fungu langu katika nchi ya walio hai.
6Sikia kuita kwangu, maana nimeshushwa chini sana; uniokoe dhidi ya watesi wangu, maana wana nguvu kuliko mimi.

Read Zaburi 142Zaburi 142
Compare Zaburi 142:1-6Zaburi 142:1-6