Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 136

Zaburi 136:17-26

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
18Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
19Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
20Na Ogu, mfalme wa Bashani, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
21Mshukuruni yeye aliyewapa nchi yao kama urithi, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
22Urithi wa Israel mtumishi wake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
23Yeye aliyetukumbuka na kutusaidia katika unyonge wetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
24Mshukuruni yeye ambaye ametupa ushindi juu ya aui zetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
25Yeye awapaye chakula viumbe hai wote, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
26Oh, mshukuruni Mungu wa mbinguni, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.

Read Zaburi 136Zaburi 136
Compare Zaburi 136:17-26Zaburi 136:17-26