Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 125

Zaburi 125:1-5

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Wale wamwaminio Yahwe ni kama mlima Sayuni, hautikisiki, wadumu milele.
2Kama milima inavyo izunguka Yerusalemu, hivyo ndivyo Yahwe anavyo wazunguka watu wake sasa na hata milele.
3Fimbo ya uovu haitatawala katika nchi ya wenye haki. Vinginevyo wenye haki wanaweza kukosea.
4Ee Yahwe, utende wema kwa wale walio wema na wale walio wanyoofu mioyoni mwao.
5Lakini kwa wale wanaogeukia njia zao za upotovu, Yahwe atawaondoa pamoja na watenda maovu. Amani iwe na Israeli.

Read Zaburi 125Zaburi 125
Compare Zaburi 125:1-5Zaburi 125:1-5