Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Zaburi - Zaburi 119

Zaburi 119:123-149

Help us?
Click on verse(s) to share them!
123Macho yangu yanachoka kwa kuusubiri wokovu wako na neno lako la haki.
124Mwoneshe mtumishi wako uaminifu wa agano lako, na unifundishe sheria zako.
125Mimi ni mtumishi wako; unipe uelewa ili niweze kuzijua amri za agano lako.
126Ni wakati wa Yahwe kutenda, kwa maana watu wamevunja sheria yako.
127Hakika ninazipenda amri zako kuliko dhahabu, naam, kuliko dhahabu safi.
128Hivyo ninayafuata maagizo yako yote kwa makini, na ninachukia kila njia ya uongo. PE.
129Sheria zako ni za ajabu, ndiyo sababu ninazitii.
130Ufafanuzi wa maneno yako huleta nuru; na kumpa ufahamu mjinga.
131Ninafungua kinywa changu na kutweta, maana ninazitamani amri zako.
132Unigeukie na unihurumie, kama ufanyavyo siku zote kwa wale walipendao jina lako.
133Uziongoze hatua zangu kwa neno lako; usiruhusu dhambi yeyote initawale.
134Unikomboe dhidi ya wanadamu waonevu ili niyatii maagizo yako.
135Uso wako umwangazie mtumishi wako, na unifundishe sheria zako.
136Mito ya machozi yatiririka kutoka machoni pangu kwa sababu watu hawaitii sheria yako. TSADHE.
137Wewe ni mwenye haki, Yahwe, na amri zako ni haki.
138Umezipa amri za agano lako haki na uaminifu.
139Hasira imeniangamiza kwa sababu adui zangu husahau maneno yako.
140Neno lako limepimwa sana, naye mtumishi wako analipenda.
141Sina umuhimu na ninadharauliwa, lakini bado siyasahau maagizo yako.
142Hukumu yako ni ya haki milele, na sheria yako ni ya kuaminika.
143Japo dhiki na taabu vimenipata, amri zako bado ni furaha yangu.
144Amri za agano lako ni za haki milele; unipe uelewa ili niweze kuishi. QOPH.
145Nililia kwa moyo wangu wote, “Unijibu, Yahwe, nitazishika sheria zako.
146Ninakuita wewe; uniokoe, nami nitazitii amri za agano lako.”
147NInaamka asubuhi kabla jua halijachomoza na kulia kwa ajili ya msaada.
148Ninatumaini katika maneno yako. Macho yangu yako wazi usiku kucha ili niweze kutafakari juu ya neno lako.
149Sikia sauti yangu katika uaminifu wa agano lako; uniweke hai, Yahwe, kama ulivyoahidi katika amri zako za haki.

Read Zaburi 119Zaburi 119
Compare Zaburi 119:123-149Zaburi 119:123-149