Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 6

Yoshua 6:12-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
12Basi Yoshua aliamka asubuhi na mapema, na makuhani wakalichukua sanduku la Yahweh.
13Makuhani saba waliobeba tarumbeta saba za pembe za kondoo waume walikuwa mbele ya sanduku la Yahweh, wakitembea kwa ushupavu, huku wakipuliza tarumbeta. Wanajeshi wenye silaha walikuwa wakitembea mbele yao, lakini walinzi wa nyuma walitembea nyuma ya sanduku la Yahweh, huku tarumbeta ziliendelea kupigwa.
14Walitembea kuuzunguka mji mara moja katika siku ya pili na kisha wakarudi kambini. Walifanya hivi kwa siku sita.
15Ilikuwa ni katika siku ya saba ambayo waliamka mapema katika mapambazuko, na walitembea kuuzunguka mji kwa namna ile kama ilivyokuwa kawaida yao, katika siku hii walifanya mara saba.
16Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, “Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahweh amewapa ninyi mji.
17Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu. Ni Rahabu yule kahaba pekee ataishi - yeye pamoja wote waliokuwa pamoja naye katika nyumba - kwasababu aliwaficha watu tuliowatuma.
18Lakini kwenu, iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu, ili baada ya kuvitia alama kwa ajili ya kuharibiwa, msichukue hata kimoja wapo. Na kama mtafanya hivi, mtaifanya kambi ya Waisraeli iharibiwe na mtaleta matatizo katika kambi.
19Fedha zote, dhahabu na vitu vilivyotengenezwa kwa shaba na chuma vilitengwa kwa ajli ya Yahweh.”
20Hivyo, watu wakapiga kelele, na wakatoa sauti kwa kupuliza tarumbeta. Ilikuwa watu waliposikia sauti za tarumbeta, walipiga kelele kwa sauti kuu, na ukuta ulianguka chini kabisa na kwamba watu waliungia mji, kila mmoja alisonga mbele moja kwa moja. Na waliuteka mji.
21Waliteketeza kabisa kila kitu kilichokuwa katika mji kwa makali ya upanga - wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, ng'ombe, kondoo na punda.
22Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, “Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwapia.”
23Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.

Read Yoshua 6Yoshua 6
Compare Yoshua 6:12-23Yoshua 6:12-23