Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 19

Yoshua 19:27-50

Help us?
Click on verse(s) to share them!
27Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
28Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
29Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
30Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
32Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
33Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
34Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
35Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
36Adama, Rama, Hazori,
37Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
38Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
39Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
40Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
41Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
42Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
43Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
44Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
45Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
46Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
47Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
48Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
49Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
50Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.

Read Yoshua 19Yoshua 19
Compare Yoshua 19:27-50Yoshua 19:27-50