Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 11

Yoshua 11:1-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Basi ikawa aliposikia haya, Yabini, mfalme wa Hazori, alituma ujumbe kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu.
2Alituma pia ujumbe kwa wafalme walikuwa katika mlima wa kaskazini mwa nchi, katika bonde la Mto Yordani kusini mwa Kinerethi, katika nchi za tambarare, na katika nchi za milima ya Dori kuelekea magharibi.
3Pia, alituma ujumbe kwa Wakanaani walioko mashariki na magharibi, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wayebusi katika nchi za milima, na Wahivi karibu na Mlima Hermoni katika nchi ya Mizipa.
4Maadui zao wote walitoka pamoja nao, wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani. Walikuwa na farasi wengi sana na magari.
5Wafalme wote hawa walikutana katika muda waliokuwa wameupanga, na walipiga kambi katika maji ya Meromu ili kupigana vita na Israeli.
6Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao.”
7Yoshua na watu wote wa vita walitoka na mara wakafika katika maji ya Meromu, na wakawashambulia maadui.
8Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli, na waliwapiga kwa upanga na wakawafuata mpaka Sidoni, Misrefothi - Maimu, na katika bonde la Mizipa upande wa mashariki. Waliwaua wote hakuna hata mmoja aliyeachwa hai.
9Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.
10Kwa wakati huo, Yoshua alirudi na akauteka mji wa Hazori. Alimwua mfalme wake kwa upanga (Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote).
11Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai. Na kisha aliuchoma moto Hazori.
12Yoshua aliiteka miji yote ya wafalme hawa. Aliwateka pia wafalme wake wote na akawapiga wote kwa upanga. Aliwateketeza kabisa kwa upanga, kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyoagiza.
13Waisraeli hawakuchoma moto mji wowote miongoni mwa miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifuasi vya udongo, isipokuwa Hazori, ndio mji pekee ambao Yoshua aliuchoma kwa moto.
14Jeshi la Israeli lilichukua nyara kutoka katika miji pamoja na mifugo kwa ajili yao wenyewe. Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai.
15Kama vile Yahweh alivyomwagiza mtumishi wake Musa, na kwa namna hiyo hiyo, Musa alivyomwagiza Yoshua. Na katika mambo yote ambayo Yahweh alimwamuru Musa kuyafanya, Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja.
16Yoshua alitwaa nchi hiyo yote, nchi ya milima, Negevu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi ya vilima vidogo, bonde la Mto Yordani, nchi ya milima ya Israeli, na nchi tambarare.
17Kutoka Mlima Halaki karibu na Edomu, kuelekea kasikazini hadi Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni chini ya Mlima Hermoni, aliwateka wafalme wake wote na kuwaua.
18Yoshua alipigana vita na wafalme wote kwa muda mrefu.
19Hakuna hata mji mmoja uliofanya amani na jeshi la Israeli isipokuwa Wahivi walioishi Gibeoni. Israeli ilitwaa miji yote iliyosalia katika vita.
20Kwa kuwa alikuwa ni Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao ili wapande na kufanya vita dhidi ya Israeli, ili kwamba aweze kuwaangamiza kabisa, na kutowaonesha huruma, kama alivyomwaagiza Musa.
21Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao.

Read Yoshua 11Yoshua 11
Compare Yoshua 11:1-21Yoshua 11:1-21