Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yoshua - Yoshua 10

Yoshua 10:1-24

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Ikawa Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alisikia kuwa Yoshua ameiteka Ai na ameiteketeza kabisa, kama alivyokwisha kufaya huko Yeriko na mfalme wake. Na alisikia jinsi ambavyo watu wa Gibeoni walivyofanya amani na watu wa Israeli na walikuwa wanaishi miongoni mwao.
2Watu wa Yerusalemu waliogopa sana kwasababu Gibeoni ulikuwa mji mkubwa, kama mmoja wa miji ya kifalme. Ilikuwa kubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa ni mashujaa wenye nguvu.
3Hivyo Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alituma ujumbe kwa Hohamu, mfalme wa Hebroni, na kwa Piramu, mfalme wa Yarimuthi, na kwaYafia, mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri, mfalme wa Eguloni:
4“Njooni kwangu na mnisaidie. Tuishambulie Gibeoni kwasababu wamefanya amani na Yoshua pamoja na watu wa Israeli.
5Wafalme watano wa Waamori; mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarimuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Eguloni walikwea, wao pamoja na majeshi yao yote. Walipanga sehemu yao kinyume na Wagibeoni na waliwashambulia.
6Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua na kwa jeshi huko Giligali. Walisema, “Upesi! Msiuondoa mkono wenu kutoka kwa watumishi wenu. Kwaeni mje haraka na mtuokoe. Mtusaide, maana wafalme wote wa Waamori wanaoishi katika nchi ya milima wamekusanyika kwa pamoja ili watushambulie.
7“Yoshua alipanda kutoka Giligali, yeye na watu wote wa vita pamoja naye, na watu wote wapiganaji.
8Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiwaogope. Nimewatiwa wote katika mkono wako. Hakuna hata mmoja wao atakayeweza kuzuia mashambulizi yako.”
9Baada ya kutembea usiku kucha kutoka Giligali, ghafla Yoshua aliwafikilia.
10Na Yahweh alichanganya maadui mbele za Israeli - ambao waliwaua mauaji makubwa mno huko Gibeoni, na wale waliowafuata njiani iendayo Bethi Horoni, nao waliuwaua katika njia iendayo Azeka na Makeda.
11Na walipokuwa wakikimbia mbio kutoka kwa Waisraeli, chini ya mlima kutoka Bethi Horoni, Yahweh alitupa mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao wote katika njia iendayo Azeka, nao wakafa. Watu waliouawa kwa mawe walikuwa ni wengi zaidi kuliko wale waliouawa kwa upanga wa watu wa Israeli.
12Kisha Yoshua akamwambia Yahweh katika siku ambayo Yahweh aliwapa watu wa Israeli ushindi dhidi ya Waamori. Hiki ndicho Yoshua alichosema kwa Yahweh mbele ya Israeli. “Jua lisimame katika Gibeoni, na mwezi, usimame katika bonde la Aijaloni.”
13Jua lilisimama, na mwezi ukaacha kwenda mpaka taifa lilipolipiza kisasi dhidi ya maadui zao. Je hili halikuandikwa katika Kitabu cha Yashari? Jua lilikaa katikati ya anga; halilkuzama kwa siku nzima hivi.
14Haijawahi kutokea siku nyingine kama hiyo kabla au baada yake, wakati Yahweh alipotii sauti ya mtu. Kwa kuwa Yahweh alikuwa akifanya vita badala ya Israeli.
15Yoshua na Israeli yote pamoja naye walirudi kambini huko Giligali.
16Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda.
17Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, “Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!”
18Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.
19Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu.”
20Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.
21Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda. Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.
22Kisha Yoshua akasema, “Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano.”
23Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.
24Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye “Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao.” Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.

Read Yoshua 10Yoshua 10
Compare Yoshua 10:1-24Yoshua 10:1-24