Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:5-18

Help us?
Click on verse(s) to share them!
5Wakati ningali ulimwenguni, mimi ni mwanga wa ulimwengu.”
6Baada ya kusema hayo, akatema mate chini, akafanyiza tope, akampaka yule kipofu machoni,
7akamwambia, “Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu.” (maana ya jina hili ni “aliyetumwa”). Basi, huyo kipofu akaenda, akanawa, kisha akarudi akiwa anaona.
8Basi, jirani zake na wale waliokuwa wanajua kwamba hapo awali alikuwa maskini mwombaji, wakasema, “Je, huyu siye yule maskini aliyekuwa akiketi na kuomba?”
9Baadhi yao wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “La! Ila anafanana naye.” Lakini huyo aliyekuwa kipofu akasema, “Ni mimi!”
10Basi, wakamwuliza, “Sasa, macho yako yalipataje kufumbuliwa?”
11Naye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka machoni na kuniambia: Nenda ukanawe katika bwawa la Siloamu. Basi, mimi nikaenda, nikanawa, nikapata kuona.”
12Wakamwuliza, “Yeye yuko wapi?” Naye akawajibu, “Mimi sijui!”
13Kisha wakampeleka huyo mtu aliyekuwa kipofu kwa Mafarisayo.
14Siku hiyo Yesu alipofanya tope na kumfumbua macho mtu huyo, ilikuwa siku ya Sabato.
15Basi, Mafarisayo wakamwuliza mtu huyo, “Umepataje kuona?” Naye akawaambia, “Alinipaka tope machoni, nami nikanawa na sasa naona.”
16Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hakutoka kwa Mungu, maana hashiki sheria ya Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Mtu mwenye dhambi awezaje kufanya ishara za namna hii?” Kukawa na mafarakano kati yao.
17Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadam yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
18Viongozi wa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwa kipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaita wazazi wake.

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:5-18Yohana 9:5-18