Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:30-41

Help us?
Click on verse(s) to share them!
30Yule mtu akajibu na kuwaambia, “Kwa nini, hili ni jambo la kushangaza, kwamba hamjui anakotoka, na bado ameyafumbua macho yangu.
31Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.
32Tangu kuanza kwa Ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote.”
34Walijibu na kumwambia, “Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?” Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.
35Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, “Unamwamini Mwana wa Mtu?”
36Alijibu na kusema, “Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?”
37Yesu akamwambia, “Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye.”
38Yule mtu akasema, “Bwana, Naamini.” Ndipo akamsujudia.
39Yesu akasema, “Kwa hukumu nimekuja katika Ulimwengu huu ili kwamba wale wasioona wapate kuona na wale wanaoona wawe vipofu.”
40Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye wakasikia maneno hayo na kumwuliza, “Na sisi pia ni vipofu?”
41Yesu akawaambia, “Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, 'Tunaona,' dhambi yenu inakaa.”

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:30-41Yohana 9:30-41