Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:21-39

Help us?
Click on verse(s) to share them!
21Lakini amepataje kuona, hatujui; na wala hatumjui yule aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima, anaweza kujitetea mwenyewe.”
22Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
23Ndiyo maana wazazi wake walisema: “Yeye ni mtu mzima, mwulizeni.”
24Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
25Yeye akajibu, “Kama ni mwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu, na sasa naona.”
26Basi, wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Alikufumbuaje macho yako?”
27Huyo mtu akawajibu, “Nimekwisha waambieni, nanyi hamkusikiliza; kwa nini mwataka kusikia tena? Je, ninyi pia mnataka kuwa wafuasi wake?”
28Lakini wao wakamtukana wakisema, “Wewe ni mfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose.
29Sisi tunajua kwamba Mungu alisema na Mose, lakini mtu huyu hatujui ametoka wapi!”
30Naye akawajibu, “Hili ni jambo la kushangaza! Ninyi hamjui ametoka wapi, lakini amenifumbua macho yangu!
31Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi, ila humsikiliza yeyote mwenye kumcha na kutimiza mapenzi yake.
32Tangu mwanzo wa ulimwengu haijasikika kwamba mtu ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.
33Kama mtu huyu hakutoka kwa Mungu, hangeweza kufanya chochote!”
34Wao wakamjibu, “Wewe ulizaliwa na kulelewa katika dhambi; unawezaje kutufundisha sisi?” Basi, wakamfukuzia mbali.
35Yesu alisikia kwamba walikuwa wamemfukuzia mbali, naye alipomkuta akamwuliza, “Je, wewe unamwamini Mwana wa Mtu?”
36Huyo mtu akajibu, “Mheshimiwa, niambie yeye ni nani, ili nipate kumwamini.”
37Yesu akamwambia, “Umekwisha mwona, naye ndiye anayesema nawe sasa.”
38Basi, huyo mtu akasema, “Ninaamini Bwana!” Akamsujudia.
39Yesu akasema, “Mimi nimekuja ulimwenguni kutoa hukumu, kusudi wasioona wapate kuona, na wale wanaoona wawe vipofu.”

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:21-39Yohana 9:21-39