Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 9

Yohana 9:17-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
17Wakamwuliza tena huyo mtu aliyekuwa kipofu, “Maadam yeye amekufungua macho, wasemaje juu yake?” Naye akawaambia, “Yeye ni nabii!”
18Viongozi wa Wayahudi hawakusadiki kwamba mtu huyo alikuwa kipofu hapo awali na sasa anaona mpaka walipowaita wazazi wake.
19Basi, wakawauliza hao wazazi, “Je, huyu ndiye mtoto wenu ambaye ninyi mwasema alizaliwa kipofu? Sasa amepataje kuona?”
20Wazazi wake wakajibu, “Tunajua kwamba huyu ni mtoto wetu, na kwamba alizaliwa kipofu.
21Lakini amepataje kuona, hatujui; na wala hatumjui yule aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima, anaweza kujitetea mwenyewe.”
22Wazazi wake walisema hivyo kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi kwani viongozi hao walikuwa wamepatana ya kwamba mtu yeyote atakayekiri kwamba Yesu ni Kristo atafukuzwa nje ya sunagogi.
23Ndiyo maana wazazi wake walisema: “Yeye ni mtu mzima, mwulizeni.”
24Basi, wakamwita tena aliyekuwa kipofu, wakamwambia, “Sema ukweli mbele ya Mungu! Sisi tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”
25Yeye akajibu, “Kama ni mwenye dhambi mimi sijui. Lakini kitu kimoja najua: Nilikuwa kipofu, na sasa naona.”
26Basi, wakamwuliza, “Alikufanyia nini? Alikufumbuaje macho yako?”
27Huyo mtu akawajibu, “Nimekwisha waambieni, nanyi hamkusikiliza; kwa nini mwataka kusikia tena? Je, ninyi pia mnataka kuwa wafuasi wake?”
28Lakini wao wakamtukana wakisema, “Wewe ni mfuasi wake; sisi ni wafuasi wa Mose.

Read Yohana 9Yohana 9
Compare Yohana 9:17-28Yohana 9:17-28