Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 8

Yohana 8:52-57

Help us?
Click on verse(s) to share them!
52Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kuwa una pepo. Abrahamu na mabii walikufa; lakini unasema, 'Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti'.
53Wewe si mkuu kuliko baba yetu Abrahamu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?”
54Yesu akajibu, “Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu.
55Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, 'simjui,' nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika.
56Baba yenu Abrahamu alishangilia atakavyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi.”
57Wayahudi wakamwambia, “Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?”

Read Yohana 8Yohana 8
Compare Yohana 8:52-57Yohana 8:52-57