Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 7

Yohana 7:13-52

Help us?
Click on verse(s) to share them!
13Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.
14Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15Wayahudi walikuwa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”
16Yesu akawajibu na kuwaambia, “Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.
17Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.
18Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.
19Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?
20Makutano wakajibu, “Una pepo. Nani anataka kukuua?”
21Yesu akajibu na akawaambia, “Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.
22Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahili mtu.
23Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?
24Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa haki.
25Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua?
26Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?
27Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.”
28Yesu alikuwa akipaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.
29Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.”
30Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.
31Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, “Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?”
32Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.
33Ndipo Yesu aliposema, “Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.
34Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja.”
35Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa Waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?
36Ni neno gani hili alilolisema, 'Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja'?”
37Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.
38Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.”
39Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.
40Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.”
41Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “nini, Kristo aweza kutoka Galilaya?
42Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?
43Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.
44Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyoosha mikono yake juu yake.
45Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?”
46Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.”
47Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa?
48Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?
49Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.”
50Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),
51“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?”
52Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.”

Read Yohana 7Yohana 7
Compare Yohana 7:13-52Yohana 7:13-52