Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 6

Yohana 6:59-71

Help us?
Click on verse(s) to share them!
59Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.
60Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili nifundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?”
61Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia je jambo hili linawakwaza?
62Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akishuka kutoka alikokuwa kabla?
63Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni roho na ni uzima.
64Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti.
65Akawambia, ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amepewa na Baba.”
66Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena.
67Yesu akawambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?”
68Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,
69na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”
70Yesu akawambia, “Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni ibilisi?
71Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.

Read Yohana 6Yohana 6
Compare Yohana 6:59-71Yohana 6:59-71