Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 6

Yohana 6:1-7

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baada ya mambo haya, Yesu alienda pande za Bahari ya Galilaya, pia huitwa Bahari ya Tiberia.
2Mkutano mkubwa ulikuwa ukimfuata kwa sababu waliona ishara alizozifanya kwa waliokuwa wagonjwa.
3Yesu alipanda juu hadi upande wa juu wa mlima na akakaa huko na wanafunzi wake
4(Na Pasaka, Sikukuu ya Wayahudi ilikuwa imekaribia).
5Yesu alipoinua macho yake juu na kuona umati mkubwa unakuja kwake, akamwambia Filipo, “Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula”?
6(Lakini Yesu aliyasema haya kwa Filipo kwa kumjaribu kwa kuwa yeye mwenyewe alijua atakachofanya).
7Filipo akamjibu, “Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo.”

Read Yohana 6Yohana 6
Compare Yohana 6:1-7Yohana 6:1-7