Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 6

Yohana 6:1-12

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa Tiberia).
2Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa.
3Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake.
4Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia.
5Basi, Yesu na alipotazama na kuona umati wa watu ukija kwake, alimwambia Filipo, “Tununue wapi mikate ili watu hawa wapate kula?”
6(Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.)
7Filipo akamjibu, “Mikate ya denari mia mbili za fedha haiwatoshi watu hawa hata kama ila mmoja atapata kipande kidogo tu!”
8Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,
9“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
10Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume elfu tano.
11Yesu akaitwaa ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia watu waliokuwa wameketi; akafanya vivyo hivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
12Watu waliposhiba Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki visipotee.”

Read Yohana 6Yohana 6
Compare Yohana 6:1-12Yohana 6:1-12