Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 5

Yohana 5:4-10

Help us?
Click on verse(s) to share them!
4Kwahiyo, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani ya baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.
5Na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane alikuwa ndani ya matao.
6Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu Yesu alimwambia, “Je unataka kuwa mzima?”
7Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapojaribu kuingia mtu mwingine hunitangulia.”
8Yesu akamwambia, “Inuka na uchukue godoro lako na uende.”
9Mara yule mtu akaponywa, akachukua kintanda chake na akaenda. Na siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
10Hivyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni siku ya Sabato, na hauruhusiwi kubeba godoro lako.”

Read Yohana 5Yohana 5
Compare Yohana 5:4-10Yohana 5:4-10