Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 5

Yohana 5:23-36

Help us?
Click on verse(s) to share them!
23ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.
24Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.
25Amini, amini, nawambia wakati unakuja na sasa upo ambao wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wote watakao sikia wataishi.
26Kwa kuwa kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake mwenyewe,
27kadhalika amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake, na Baba amempa Mwana mamlaka ili kwamba ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.
28Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
29nao watatoka nje: kwa waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
30Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
31Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
32Kuna mwingine anayeshuhudia kuhusu mimi na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
33Mmetuma kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
34Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
35Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
36Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.

Read Yohana 5Yohana 5
Compare Yohana 5:23-36Yohana 5:23-36