Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 5

Yohana 5:16-23

Help us?
Click on verse(s) to share them!
16Kwa vile Yesu alifanya jambo hilo siku ya Sabato, Wayahudi walianza kumdhulumu.
17Basi, Yesu akawaambia, 鈥淏aba yangu anafanya kazi daima, nami pia nafanya kazi.鈥
18Kwa sababu ya maneno haya, viongozi wa Wayahudi walizidi kutafuta njia ya kumwua Yesu: si kwa kuwa aliivunja Sheria ya Sabato tu, bali pia kwa kuwa alisema kwamba Mungu ni Baba yake, na hivyo akajifanya sawa na Mungu.
19Yesu akawaambia, 鈥淜weli nawaambieni, Mwana hawezi kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya. Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.
20Baba ampenda Mwana, na humwonyesha kila kitu anachokifanya yeye mwenyewe, tena atamwonyesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.
21Kama vile Baba huwafufua wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo naye Mwana huwapa uzima wale anaopenda.
22Baba hamhukumu mtu yeyote; shughuli yote ya hukumu amemkabidhi Mwana,
23ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba ambaye amemtuma.

Read Yohana 5Yohana 5
Compare Yohana 5:16-23Yohana 5:16-23