Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 5

Yohana 5:11-43

Help us?
Click on verse(s) to share them!
11Akajibu, yeye aliyeniponya ndiye aliyeniambia, “Chukua godoro lako na uende.”
12Wakauliza, “Ni nani aliyekuambia 'Chukua godoro lako na uende?'''
13Ingawa, yule aliyeponywa hakumjua, kwa sababu Yesu alikuwa ameondoka kwa siri. Kwa kuwa kulikuwa na watu wengi katika sehemu hiyo.
14Baada ya hapo Yesu alimkuta yule mtu hekaluni na akamwambia, “Tazama, umepona! “Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi.”
15Yule mtu akaenda na kuwataarifu Wayahudi kuwa Yesu ndiye aliyemponya.
16Hivyo, kwa sababu ya mambo hayo Wayahudi walimtesa Yesu, kwa sababu alifanya mambo haya siku ya Sabato.
17Yesu akawambia, “Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami nafanya kazi.”
18Kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kumtafuta ili wamuue sio tu kwa sababu ya kuivunja Sabato, bali kwa kumwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.
19Yesu akawajibu, “Amini, amini, Mwana hawezi kufanya kitu chochote isipokuwa kile ambacho amemwona Baba yake anakifanya, kwa kuwa chochote Baba akifanyacho ndicho na Mwana atakachofanya.
20Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, na amwonyesha kila kitu anachokifanya na atamwonyesha mambo makubwa kuliko haya ili kwamba mzidi kushangaa.”
21Kwa kuwa kama vile ambavyo Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, halikadhalika Mwana pia humpa yeyote ampendaye.
22Kwa kuwa Baba hamhukumu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote
23ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.
24Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.
25Amini, amini, nawambia wakati unakuja na sasa upo ambao wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wote watakao sikia wataishi.
26Kwa kuwa kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake mwenyewe,
27kadhalika amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake, na Baba amempa Mwana mamlaka ili kwamba ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.
28Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake
29nao watatoka nje: kwa waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
30Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.
31Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.
32Kuna mwingine anayeshuhudia kuhusu mimi na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.
33Mmetuma kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.
34Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.
35Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.
36Ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.
37Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.
38Hamna neno lake likikaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.
39Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na
40hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.
41Sipokei sifa kutoka kwa watu,
42lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.
43Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.

Read Yohana 5Yohana 5
Compare Yohana 5:11-43Yohana 5:11-43