Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 4

Yohana 4:45-54

Help us?
Click on verse(s) to share them!
45Alipokuja kutoka Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.
46Alikuja tena Kana ya Galilaya huko alikoyabadilisha maji kuwa divai. Palikuwa na ofisa ambaye mwana wake alikuwa ni mgonjwa huko Kapernaumu.
47Aliposikia kuwa Yesu alitoka Judea na kwenda Galilaya, alienda kwa Yesu na kumsihi atelemke amponye mwanawe, ambaye alikuwa karibu kufa.
48Ndipo Yesu akamwambia, “Ninyi msipoona ishara na maajabu hamwezi kuamini.
49Kiongozi akasema, “Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa.”
50Yesu akamwambia, “Nenda mwanao ni mzima.” Yule mtu akaamini neno alilolisema Yesu na akaenda zake.
51Alipokuwa akishuka, watumishi wake walimpokea na kumwambia mwana wake alikuwa mzima.
52Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, “Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha.”
53Ndipo baba yake akatambua kuwa ni muda ule ule Yesu aliosema, “Mwana wako ni mzima.” Hivyo yeye na familia yake wakaamini.
54Hii ilikuwa ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipotoka Yudea kwenda Galilaya.

Read Yohana 4Yohana 4
Compare Yohana 4:45-54Yohana 4:45-54