Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 4

Yohana 4:35-44

Help us?
Click on verse(s) to share them!
35Je, hamsemi, 'Bado miezi mitano na mavuno yatakuwa tayari?' Ninawambieni tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno!
36Yeye avunaye hupokea mishahara na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.
37Kwa kuwa msemo huu ni wa kweli, 'Mmoja apanda na mwingine avuna.'
38Niliwatuma kuvuna ambacho hamkukihangaikia, Wengine wamefanya kazi na ninyi mmeingia katika furaha ya kazi yao.”
39Wasamaria wengi katika mji ule walimwani kwa sababu ya taarifa ya yule mwanamke aliyekuwa akishuhudia, “Aliyeniambia mambo yote niliyoyafanya.”
40Hivyo Wasamaria walipokuja walimsihi akae pamoja nao na akakaa kwao kwa siku mbili.
41Na wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.
42Wakamwambia yule mwanamke, “Tunaamini sio tu kwa maneno yako, kwa sababu sisi wenyewe tumesikia, na sasa twafahamu kuwa hakika yeye ni mwokozi wa ulimwengu.”
43Baada ya siku hizo mbili, akaondoka na kuelekea Galilaya.
44Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe.

Read Yohana 4Yohana 4
Compare Yohana 4:35-44Yohana 4:35-44