Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 4

Yohana 4:33-50

Help us?
Click on verse(s) to share them!
33Wanafunzi wake wakaulizana, “Je, kuna mtu aliyemletea chakula?”
34Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.
35Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.
36Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.
37Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna.
38Mimi nimewatuma mkavune mavuno ambayo hamkuyatolea jasho, wengine walifanya kazi, lakini ninyi mnafaidika kutokana na jasho lao.”
39Wasamaria wengi wa kijiji kile waliamini kwa sababu ya maneno aliyosema huyo mama: “Ameniambia mambo yote niliyofanya.”
40Wasamaria walimwendea Yesu wakamwomba akae nao; naye akakaa hapo siku mbili.
41Watu wengi zaidi walimwamini kwa sababu ya ujumbe wake.
42Wakamwambia yule mama, “Sisi hatuamini tu kwa sababu ya maneno yako; sisi wenyewe tumesikia, na tunajua kwamba huyu ndiye kweli Mwokozi wa ulimwengu.”
43Baada ya siku mbili Yesu aliondoka hapo, akaenda Galilaya.
44Maana Yesu mwenyewe alisema waziwazi kwamba, “Nabii hapati heshima katika nchi yake.”
45Basi, alipofika Galilaya, Wagalilaya wengi walimkaribisha. Maana nao pia walikuwa kwenye sikukuu ya Pasaka, wakayaona mambo yote Yesu aliyotenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu hiyo.
46Yesu alifika tena huko mjini Kana, mkoani Galilaya, mahali alipogeuza maji kuwa divai. Kulikuwa na ofisa mmoja aliyekuwa na mtoto mgonjwa huko Kafarnaumu.
47Basi, huyo ofisa aliposikia kuwa Yesu alikuwa ametoka Yudea na kufika Galilaya, alimwendea akamwomba aende kumponya mtoto wake aliyekuwa mgonjwa mahututi.
48Yesu akamwambia, “Msipoona ishara na maajabu hamtaamini!”
49Huyo ofisa akamwambia, “Mheshimiwa, tafadhali twende kabla mwanangu hajafa.”
50Yesu akamwambia, “Nenda tu, mwanao yu mzima.” Huyo mtu akaamini maneno ya Yesu, akaenda zake.

Read Yohana 4Yohana 4
Compare Yohana 4:33-50Yohana 4:33-50