Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 4

Yohana 4:23-37

Help us?
Click on verse(s) to share them!
23Lakini wakati unakuja, tena umekwisha fika, ambapo wanaoabudu kweli, watamwabudu Baba kwa nguvu ya Roho; watu wanaomwabudu hivyo ndio Baba anaotaka.
24Mungu ni Roho, na watu wataweza tu kumwabudu kweli kwa nguvu ya Roho wake.”
25Huyo mama akamwambia, “Najua kwamba Masiha, aitwaye Kristo, anakuja. Atakapokuja atatujulisha kila kitu.”
26Yesu akamwambia, “Mimi ninayesema nawe, ndiye.”
27Hapo wanafunzi wake wakarudi, wakastaajabu sana kuona anaongea na mwanamke. Lakini hakuna mtu aliyesema: “Unataka nini?” au, “Kwa nini unaongea na mwanamke?”
28Huyo mama akauacha mtungi wake pale, akaenda mjini na kuwaambia watu,
29“Njoni mkamwone mtu aliyeniambia mambo yote niliyotenda! Je, yawezekana kuwa yeye ndiye Kristo?”
30Watu wakatoka mjini, wakamwendea Yesu.
31Wakati huohuo wanafunzi wake walikuwa wanamsihi Yesu: “Mwalimu, ule chakula.”
32Lakini Yesu akawaambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.”
33Wanafunzi wake wakaulizana, “Je, kuna mtu aliyemletea chakula?”
34Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya anachotaka yule aliyenituma na kuitimiza kazi yake.
35Ninyi mwasema: Bado miezi minne tu, na wakati wa mavuno utafika! Lakini mimi nawaambieni, yatazameni mashamba; mazao yako tayari kuvunwa.
36Mvunaji anapata mshahara wake, na anakusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele; hivyo mpandaji na mvunaji watafurahi pamoja.
37Kwa sababu hiyo msemo huu ni kweli: Mmoja hupanda na mwingine huvuna.

Read Yohana 4Yohana 4
Compare Yohana 4:23-37Yohana 4:23-37