Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 3

Yohana 3:23-28

Help us?
Click on verse(s) to share them!
23Yohane pia alikuwa akibatiza watu huko Ainoni, karibu na Salemu, maana huko kulikuwa na maji mengi. Watu walimwendea, naye akawabatiza.
24(Wakati huo Yohane alikuwa bado hajafungwa gerezani.)
25Ubishi ulitokea kati ya baadhi ya wanafunzi wa Yohane na Myahudi mmoja kuhusu desturi za kutawadha.
26Basi, wanafunzi hao wakamwendea Yohane na kumwambia, “Mwalimu, yule mtu aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani na ambaye wewe ulimshuhudia, sasa naye anabatiza, na watu wote wanamwendea.”
27Yohane akawaambia, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu.
28Nanyi wenyewe mwaweza kushuhudia kuwa nilisema: Mimi siye Kristo, lakini nimetumwa ili nimtangulie!

Read Yohana 3Yohana 3
Compare Yohana 3:23-28Yohana 3:23-28