Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 3

Yohana 3:1-11

Help us?
Click on verse(s) to share them!
1Kulikuwa na kiongozi mmoja Myahudi, wa kikundi cha Mafarisayo, jina lake Nikodemo.
2Siku moja alimwendea Yesu usiku, akamwambia, “Rabi, tunajua kwamba wewe ni mwalimu uliyetumwa na Mungu, maana hakuna mtu awezaye kufanya ishara unazozifanya Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3Yesu akamwambia, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa upya hataweza kuuona ufalme wa Mungu.”
4Nikodemo akamwuliza, “Mtu mzima awezaje kuzaliwa tena? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake na kuzaliwa mara ya pili!”
5Yesu akamjibu, “Kweli nakwambia, mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kamwe kuingia katika ufalme wa Mungu.
6Mtu huzaliwa kimwili kwa baba na mama, lakini huzaliwa kiroho kwa Roho.
7Usistaajabu kwamba nimekwambia kuwa ni lazima kuzaliwa upya.
8Upepo huvuma kuelekea upendako; waisikia sauti yake, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyezaliwa kwa Roho.”
9Nikodemo akamwuliza, “Mambo haya yanawezekanaje?”
10Yesu akamjibu, “Je, wewe ni mwalimu katika Israel na huyajui mambo haya?
11Kweli nakwambia, sisi twasema tunayoyajua na kushuhudia tuliyoyaona, lakini ninyi hamkubali ujumbe wetu.

Read Yohana 3Yohana 3
Compare Yohana 3:1-11Yohana 3:1-11