Text copied!
CopyCompare
Biblia ya Kiswahili - Yohana - Yohana 2

Yohana 2:18-25

Help us?
Click on verse(s) to share them!
18Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?”
19Yesu akawajibu, libomoeni Hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.”
20Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Iligharimu miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?”
21Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.
22Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.
23Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa Pasaka, wakati wa sikukuu watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya.
24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote.
25Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.

Read Yohana 2Yohana 2
Compare Yohana 2:18-25Yohana 2:18-25