Text copied!
CopyCompare
Biblia Takatifu - Yohana - Yohana 2

Yohana 2:14-21

Help us?
Click on verse(s) to share them!
14Hekaluni aliwakuta watu wakiuza ng'ombe, kondoo na njiwa, na wavunja fedha walikuwa wamekaa kwenye meza zao.
15Akatengeneza mjeledi wa kamba, akawafukuza wote nje ya Hekalu pamoja na kondoo na ng'ombe wao, akazimwaga sarafu za wenye kuvunja fedha na kupindua meza zao.
16Akawaambia wale waliokuwa wanauza njiwa, “Ondoeni vitu hivi hapa. Msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa soko!”
17Wanafunzi wake wakakumbuka kwamba Maandiko yasema: “Upendo wangu kwa nyumba yako waniua.”
18Baadhi ya Wayahudi wakamwuliza Yesu, “Utafanya muujiza gani kuonyesha kwamba unayo haki kufanya mambo haya?”
19Yesu akawaambia, “Vunjeni Hekalu hili, nami nitalijenga kwa siku tatu.”
20Hapo Wayahudi wakasema, “Hekalu hili lilijengwa kwa muda wa miaka arobaini na sita. Je, wewe utalijenga kwa siku tatu?”
21Lakini Yesu alikuwa anaongea juu ya Hekalu ambalo ni mwili wake.

Read Yohana 2Yohana 2
Compare Yohana 2:14-21Yohana 2:14-21